Home
Links
Bible Versions
Contact
About us
Impressum
Site Map


WoL AUDIO
WoL CHILDREN


Bible Treasures
Doctrines of Bible
Key Bible Verses


Afrikaans
አማርኛ
عربي
Azərbaycanca
Bahasa Indones.
Basa Jawa
Basa Sunda
Baoulé
বাংলা
Български
Cebuano
Dagbani
Dan
Dioula
Deutsch
Ελληνικά
English
Ewe
Español
فارسی
Français
Gjuha shqipe
հայերեն
한국어
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
Кыргызча
Lingála
മലയാളം
Mëranaw
မြန်မာဘာသာ
नेपाली
日本語
O‘zbek
Peul
Polski
Português
Русский
Srpski/Српски
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
ไทย
Tiếng Việt
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Uyghur/ئۇيغۇرچه
Wolof
ייִדיש
Yorùbá
中文


ગુજરાતી
Latina
Magyar
Norsk

Home -- Kiswahili -- John - 031 (Jesus leads his disciples to see the ready harvest; Evangelism in Samaria)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
C - Kristo kutembelea mara ya kwanza mji wa Yerusalemu (Yohana 2:13 - 4:54) -- Neno Kuu: Kuabudu kwa kweli ni nini?
4. Yesu atembelea Samaria (Yohana 4:1–42)

b) Yesu awaongoza wanafunzi wake waone mavuno yaliyo tayari (Yohana 4:27-38)


YOHANA 4:31-38
31 “Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema: Rabi, ule; 32 akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi. 33 Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je, mtu amemletea chakula? 34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake. 35 Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno. 36 Naye avunaye hupokea mshahara, na kukusanya matunda kwa uzima wamilele, ili yeye apandaye na yeye avunaye wapate kufurahi pamoja. 37 Kwa maana hapo neno hilo huwa kweli: Mmoja hupanda akavuna mwingine. 38 Mimi naliwatuma myavune yale msioyataabikia; wengine walitaabika nanyi mmeingia katika taabu yao”

Baada ya Yesu kuokoa roho ya yule mama mzinzi na kumwongoza kwa uzima wa milele, aliwaelekea wanafunzi wake ili kuwapatia pia huduma iliyofanana. Mawazo yao yalikawia kuwa ya kidunia kuhusu mambo ya kawaida. Hawakuchangamka kwa habari ya mambo ambayo Roho wa Mungu alifanya moyoni mwa yule mwanamke.

Kwa kweli, chakula na kinywaji ni lazima ili tuishi, lakini kuna chakula muhimu zaidi kuliko mkate, na inaridhisha vizuri zaidi kuliko maji ya kunywa. Hilo bado walihitaji kutambua vizuri. Wao walikuwa si bora kuliko yule mwanamke, ingawa walijifunga kumfuata Yesu.

Yesu aliwaelezea maana ya chakula cha mbinguni au cha kiroho. Hiki kinaridhisha roho zetu zaidi kuliko chakula cho chote cha kawaida. Yesu mwenyewe alikuwa ameridhika kabisa kwa kumzawadia fulani baraka na kutenda mapenzi ya Baba yake.

Yesu alikuwa ni mtume wa Mungu. Alikuwa ni mwanaye huru kabisa, hata hivyo mtii kabisa kwa babaye, akitimiza mapenzi yake kwa furaha, maana Mungu ni upendo. Yeyote aishiye katika upendo, anaishi ndani ya Mungu. Utiifu wa Kristo haimaanishi kwamba alikuwa chini ya Baba, ila inathibitisha ukamilifu wa upendo wake kwake. Mwana alitamka kwamba, wokovu wa ulimwengu ni kazi ya Baba yake, iwapo aliikamilisha yeye mwenyewe. Alimpa Baba utukufu yote, jinsi Baba kabla ya hapo alikabidhi mambo yote kwake Mwana. Baba anampatia ukuu Mwana wake na kumketisha mkono wake wa kulia, akimwekea enzi yote mbinguni na duniani mkononi mwake.

Pale kisimani mapenzi ya Mungu ilikuwa kumwokoa yule mwanamke mdharauliwa. Haikuwa kwamba Wayahudi tu waitwe kuokolewa, lakini binadamu wote. Wote walikuwa wamepevuka, wakiwa na njaa kwa Mungu. Yesu kwa kukutana na huyu mama, alikuta ndani yake mambo hayo kamili: njaa kwa kusamehewa na kukubalika tena kwa utu wake wa ndani. Utayari wa kupokea uradhi wa Mungu ilikuwa wazi zaidi ndani yake kuliko ndani ya wengi wa Wayahudi. - Ndipo kwa ghafula Yesu aliona mbele yake ubinadamu wote kama shamba kubwa likijaa ngano nyeupe, tayari kwa kuvunwa, likipulizwa na upepo kwa Roho Mtakatifu.

Hata hivyo, wanafunzi hawakuweza kuona picha hii ya shamba, ikimaanisha ulimwengu ulivyo tayari kwa mavuno. Yesu alifikia hapo Samaria wakati kabla ya msimu wa kupanda, na ilihitajika miezi kadhaa kabla ya kutokeza mavuno. Ilikuwa kana kwamba Yesu alisema: Ninyi mnaangalia mambo kwa juu-juu yalivyo kawaida. Tazameni kwenye ukweli ndani ya kiini cha roho za watu; maswali magumu yakiwakandamiza, hamu kubwa kwa maisha ya kweli na kumtafuta Mungu hasa. Basi LEO ni wakati wa kuvuna! Wako wengi wenye kutamani kumkubali Mwana wa Mungu kuwa mwokozi wao, kama ujumbe wa wokovu unaelezwa kwao kwa hekima na upendo.

Pengine, ndugu, unasikia tofauti: wote hao wanaonizunguka hawana akili, ni washupavu au vipofu. Basi Yesu aliwatambua hadi mioyoni. Hakumhukumu yule mama mwenye maisha machafu, aliyeongea naye kwanza kama mgeni. Hakusita kuzungumza naye, ingawa mambo ya kiroho yalikuwa yanampita, basi akaongea naye maneno ya wazi na rahisi. Hivyo akamsaidia zaidi kwa uongozi wa Roho, akaamsha ndani yake kumbukumbu za kuabudu na ukuu wa mtazamo wa Masihi, hadi hapo alipopata kuwa mwinjilisti mwenyewe. Badiliko kuu ya namna gani! Huyu alifikia karibu zaidi huduma ya Roho kuliko mtu wa dini Nikodemo. Kila mtu anayemtumikia Bwana anahitaji kujaliwa mtazamo wa ndani ya watu mwenye upendo kama Yesu, ili kuwatambua wenye njaa kwa haki ya Mungu ndani ya uaminifu wao. Usihangaike kwa ajili ya kukwaruzwa nao au wasiwasi wao; Mungu anawapenda, Bwana Yesu anawaita. Mawazo yao yatatiwa nuru pole pole kwa neema. Hadi lini wewe utakaa kimya katika ulimwengu unaojaa wenye kumtafuta Mungu?

Wakati mtu anaporudi kwa Kristo, uzima wa milele itakuwa wake; furaha itajaa mioyo ya wengi. Hata mbinguni kutakuwa na furaha kuu kwa malaika kwa ajili ya mmoja mwenye dhambi anapotubu. Pamoja na hayo ni hamu ya Mungu kuwaokoa wote na kufikia ufahamu wa ukweli. Wale watu wanaoambatana na mapenzi hayo ya Mungu na kuyapeleka mbele kwa kuhubiri kwa wengine, kwa unyenyekevu wataridhisha roho zao na kufurahi. Jinsi Yesu alivyosema kwa ajili yake mwenyewe: “Chakula changu ni kutenda kazi ya yule aliyenipeleka na kutimiza mapenzi yake”. Yesu alimalizia ujumbe wake kwa wanafunzi wake akisema: “Mimi nawatuma ili mvune.” Mbatizaji alikuwa amelima sana mashamba ya kame akihubiri toba - Yesu mwenyewe analingana na mbegu ya ngano, ambayo Mungu aliipanda ndani ya ardhi iliyokuwa imetayarishwa. - Sisi siku hizi tunavuna matunda ya kifo chake msalabani. Ikiwa Yesu anakuita kwenye kazi ya mavuno, kumbuka kwamba mavuno sio yako. Kwa vyovyote kazi ni ya Bwana. Nguvu ya Kristo inaivisha matunda ya kiroho. Sisi sote tu watumishi tusiofaa, hata hivyo anatuita kushiriki katika huduma yake tukufu, wakati mwingine kwa kupanda, wakati mwingine kwa kulima au pia kwa kuvuna. Ni vema tukumbuke kwamba, sisi sio wafanya kazi wa kwanza wa Mungu. Wengi walihangaika kabla yetu, hata kwa machozi; sala zao zimeandikwa mbinguni. Wewe hujatayarishwa bora kuliko watumishi wengine wa Mungu, wala huna namna bora kuliko wengine. Kila dakika unaishi na uradhi wa rehema zake tu. Basi, jifunza kumtii Roho kwenye huduma yako. Umtumikie kwa kumsifu na shukrani wakati wa mavuno. Mtukuze Baba yako wa mbinguni pamoja na wavunaji wengine mkilia: “Ufalme wako uje - enzi yote ni yako, nguvu na utukufu milele, Amina”.


c) Uinjilisti kule Samaria (Yohana 4:39-42)


Yohana 4:39-42
39 “Na katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini wengi kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda. 40 Basi wale wasamaria walipomwendea, walimsihi akae kwao; naye akakaa huko siku mbili. 41 Watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu ya neno lake. 42 Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu; maana sisi tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu.”

Umati wa watu walimkimbilia Yesu toka mjini baada ya kuvutwa na maongezi ya yule mama. Ndani ya hao Yesu aliona shamba nyeupe, karibu kuiva kwa mavuno. Alisema nao habari ya imani na uzima wa milele, akakaa pale siku mbili nzima. Wanafunzi wake walitembelea nyumba zao kama wavunaji wa roho za watu. Mamlaka yake Kristo na maneno yake yakagusa sana hao watu wengi. Walitambua kwamba Mungu alijia ulimwengu wa shida ndani ya Kristo, ili aokoe wenye dhambi. Hao Wasamaria ndio wa kwanza wa kumwita “Mwokozi wa ulimwengu”. Walisikia kwamba Yesu hakukusudia kuokoa watu wake wenyewe tu, bali kwamba alijitwisha makosa ya watu wote. Walitambua hakuna mwisho kwa nguvu ya upendo wake; hata leo anaweza kuokoa na kuweka huru wale wenye mapingu ya dhambi kwa mshiko wa Shetani, na zaidi anawalinda wale waliokwisha kuwekwa huru. Yeye kweli ni hakimu wa ulimwengu. – Kaisari kule Rumi alipewa cheo cha “Mwokozi na Mtunzaji wa dunia”. Ila hao Wasamaria walitambua kwamba Yesu ni mkuu kuliko Makaisari; maana anawapa watu wake amani ya milele.

SALA: Tunakushukuru, Yesu; ulijenga kwa upya maisha ya yule mama mwenye dhambi, na kutuonyesha na sisi sote kwamba, utiifu ni bora kuliko kuabudu. Utuweke huru na kuchelewa kwetu, ili tuweze kutimiza mapenzi yako haraka na kwa furaha, tukitolea wokovu wako kwa wadhululaji, ili nao wapokee uhai wa milele kwa njia ya imani ndani yako.

SWALI:

  1. Jinsi gani tutapata kuwa wavunaji wa kufaa kwa ajili ya Yesu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:58 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)