Home
Links
Bible Versions
Contact
About us
Impressum
Site Map


WoL AUDIO
WoL CHILDREN


Bible Treasures
Doctrines of Bible
Key Bible Verses


Afrikaans
አማርኛ
عربي
Azərbaycanca
Bahasa Indones.
Basa Jawa
Basa Sunda
Baoulé
বাংলা
Български
Cebuano
Dagbani
Dan
Dioula
Deutsch
Ελληνικά
English
Ewe
Español
فارسی
Français
Gjuha shqipe
հայերեն
한국어
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
Кыргызча
Lingála
മലയാളം
Mëranaw
မြန်မာဘာသာ
नेपाली
日本語
O‘zbek
Peul
Polski
Português
Русский
Srpski/Српски
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
ไทย
Tiếng Việt
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Uyghur/ئۇيغۇرچه
Wolof
ייִדיש
Yorùbá
中文


ગુજરાતી
Latina
Magyar
Norsk

Home -- Kiswahili -- John - 109 (The choice; The flogging of Jesus; Pilate awed by Christ)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 4 - Nuru Inashinda Giza (Yohana 18:1 - 21:25)
A - Matokeo kuanzia kukamatwa kwake Yesu hadi kuzikwa kwake (Yohana 18:1 - 19:42)
3. Kesi ya kiserikali mbele ya mtawala wa kirumi (Yohana 18:1 - 19:42)

b) Uchaguzi kati ya Yesu na Baraba (Yohana 18:39–40)


Yohana 18:39-40
“Lakini kwenu kuna desturi ya mimi kuwafungulia mtu mmoja wakati wa Pasaka; basi mwapenda niwafungulie Mfalme wa Wayahudi? Basi wakapiga kelele tena kusema, Si huyu , bali Baraba. Naye yule Baraba alikuwa mnyang’anyi”

Pilato aliamini kabisa kwamba Yesu ni mwaminifu wala haleti hatari yoyote. Aliwatokea Wayahudi waliomngojea nje uani, ndipo alishuhudia hadharani kwamba mstakiwa hana hatia. Injili zote nne zinahakikisha kwamba Yesu aliishi bila lawama yoyote mbele ya amri ya torati na pia mbele ya sheria za nchi. Akiwa mtawala hakuweza kuona hatia hata moja juu ya Yesu. Hivyo msimamizi wa mamlaka ya serikali akathibitisha kwamba Yesu hana kosa. Pilato alipenda kumwondoa huyu mgeni mbele zake, lakini upande mwingine alijibidiisha kuwapendekeza Wayahudi. Alipendekeza kumfungulia mfungwa fulani kwa sababu ya desturi zao kumruhusu mmoja wa washtakiwa kwa kumsamehe sikukuu ya Pasaka. Alijaribu kumridhisha kuhani mkuu kwa kumwita Yesu “Mfalme wa Wayahudi” kwa dhihaka. Kama Pilato angemruhusu, Yesu angepoteza sifa yake kwa watu (ndivyo Pilato alivyotetea), maana hakuweza kuwaweka huru watu wake kutoka kwa utumwa wa Warumi.

Hata hivyo, makuhani na mati ya watu wakachafuka kwa kusikia “Mfalme wa Wayahudi”. Walikuwa wamemtazamia mwenye enzi ya kijeshi, mwenye mamlaka na mkali. Basi wakamchagua Baraba mnyang’anyi; hivyo kumpendekeza mtu wa hatia, mbali na Mtakatifu wa Mungu.

Sio baraza tu iliyokuwa kumpinga Yesu, lakini pia na mati ya watu waliomdharau. - Wewe je, utasimama imara pamoja na kweli, na wanyenyekevu na wasio na silaha, au utafanana na hao wenye sheria, waliotegemea vurugo au udanganyifu, mbali sana na sifa hizo za huruma na ukweli?


c) Kupigwa kwake Yesu mbele za washitaki wake (Yohana 19:1-5)


Yohana 19:1-3
“Basi ndipo Pilato alipomtwaa Yesu, akampiga mijeledi. Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau. Wakawa wakimwekea, wakisema, Salamu! Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi.”

Ilimpasa Pilato kumpatia Yesu uhuru na kuwafunga washitaki. Hilo hakfanya, badala yake akageuza mambo na kutafuta namna ya kuridhiana. Basi akaagiza Yesu apigwe. Kuadhibiwa namna hii ilikuwa ya kutisha na kuchosha sana. Ile mijeledi ilifungiwa vipande vya mifupa kwenye ncha zake zilizokata ndani ya ngozi. Wakati askari walipomsumbua Yesu kwa mashitusho, wakamfunga mgongo uchi kwenye nguzo na kumswaga mapigo mwilini mwake. Ngozi na nyama yake zilijeruhiwa mno na kumpatia maumivu yasiosemeka. Wengine walikuwa wanakufa kwa kushughulikiwa namna hii. Bwana wetu aliyekuwa bila kosa lolote alivumilia mengi sana mwilini na rohoni.

Ndipo askari, kwa kuendeleza dhihaka, wakachukua mwili wa Yesu uliojeruhiwa hivyo. – Hao askari waliishi wakihofia fujo za Wayahudi, hata wasijaribu kutembea nje kwa usiku. Hapo basi wakaona nafasi yao ya kufaa kujilipiza kwa kumtesa fulani aliyejiita “Mfalme wa Wayahudi” - Hivyo ukorofi wao wote waliosikia juu ya hao watu wenye fujo ulimwagwa juu yake. Mmojawao akakimbia na kuvunja tawi kwenye kichaka cha miiba, akaivingirisha kwa namna ya taji na kuiweka kenye kichwa cha Kristo. Shindilio la taji hilo la miiba lilitokeza damu kutiririka usoni. Wengine wakaja na nguo zilizotumika na ofisa fulani, wakamvisha. Damu ikachanganyika na uwekundu wa rangi yaa nguo, hadi Yesu akaonekana amefunikwa na damu tupu. Juu ya hayo yote alipigwa mateke na kuchomwa kikorofi. Hata wengine wakainama mbele zake, kana kwamba wanamheshimu kwa sababu ya kuwekewa taji la kifalme. Huenda vikosi hivi kutoka maeneo yote ya utawala wa kirumi vilitokana na mataifa kadhaa ya kiulaya, hivyo basi makabila mengi ya dunia yetu yalishiriki katika dhihaka na unajisi huo na kuilenga kwa Mwana Kondoo wa Mungu.

Yohana 19:4-5
“Kisha Pilato akatokea tena nje, akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa mimi sioni hatia yo yote kwake. Nipo Yesu alipotoka nje, naye amevaa ile taji ya miiba, na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia,Tazama, Mtu huyu!”

Pilato akachunguza tena maandiko ya mashitaka dhidi ya Yesu, naye akaona kwamba hana hatia. Basi kwa mara ya tatu akaenda nje kwa viongozi wa Wayahudi na kushuhudia tena, “Mimi sioni hatia yoyote kwa huyu mtu.” Mwishowe basi, akajaribu kuwaleta pamoja uso kwa uso, ili ifunuliwa udanganyifu na ukweli udhihirishwe.

Alimleta Yesu nje tena, akiwa na alama zote za mapigo na machozi na damu ikitiririka kwa wingi, pia na taji ya miiba kwenye paji la uso. Begani mwake ilionekana lile vazi la zambarau lililochujwa na damu.

Unaweza kuona sura ya Mwana Kondoo wa Mungu akibeba dhambi za ulimwengu ? Udhihilifu wake ilikuwa heshima ya kuinuliwa, maana upendo wake usiosemeka ilionekana katika ustahimilivu wake. - Alisimama mbele ya wale walioshiriki kwa niaba ya Mashariki na Magharibi, wakimdharau, wakimwonea na kumvisha miiba kichwani. Taji zote za dunia hii pamoja na marumaru za kungaa na dhahabu hazina thamani kwa kulinganisha na taji lake la miiba pamoja na damu yake inayolipia dhambi zote.

Ingawa Pilato alikuwa ni mtu mshupavu sana kabla ya hapo, akaguswa sana na picha hii. Haikuwepo dalili yoyote ya chuki usoni mwake Yesu, wala laana mdomoni mwake. Aliomba kimya kwa Baba yake, akawabariki adui zake na kubeba dhambi za wale waliomtukana. Mtawala huyu akatamka maneno hayo ya kugusa: “Tazama, mtu huyu!” Alitambua enzi na adhama ya mtu huyu. Kana kwamba alitaka kusema habari ya Kristo: “Huyu ni mtu wa pekee abebaye sura ya mungu.” Rehema zake ilienea hata saa hiyo ya hatari ya kufa; utukufu wake uling’aa katika unyenyekevu wake na mwili wake ulioathiriwa namna hii. Yeye hakuvumilia kwa ajili ya matendo yake mabaya, bali kwa ajili ya dhambi zangu na za kwako, pamoja na hatia ya binadamu .


d) Pilato aliogofya kwa hali tukufu ya Kristo (Yohana 19:6–12)


Yohana 19:6-7
„Basi wale wakuu wa makuhani na watumishi wao walipomwona, walipiga kelele wakisema, Msulibishe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi basi, mkamsulibishe; maana mimi sioni hatia kwake. Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu.“

Masaa ya mateso yalikuwa marefu, na wengi kati ya umati wa watu walitelemkia kwenye malango ya jumba la mtawala. Uongozi wa kiyahudi walikataa kabisa kulegeza makusudi yao wala kuona huruma, lakini walikuwa wameafikiana kudai kifo chake Yesu mara moja, wakiwa wana paza sauti zao na kufanya fujo kuu.. Wale walioelekea kuwa na huruma wakatiwa hofu na kukata tamaa na pengine kuhisi kwamba Mungu amemwacha Yesu. Yeye hakuwapatia mwujiza wa kujiokoa, na hivyo madai ya kutimiliza yakakua, na wakamtazamia Pilato apitishe hukumu iliyo kali kuliko yote. Hivyo wakamdhalilisha na kumtupia shimoni mwa aibu.

Wakati huo basi, Pilato akawa macho sana kwa dalili yoyote ya machafuko kati ya mati, hata hivyo hakupenda kumwua fulani kinyume cha sheria. Basi akawaambia Wayahudi, „Mchukueni na kumsulibisha, ingawa mimi nimehakikisha kwamba hana hatia“ - na hii ni mara ya tatu kwamba amekir yai kwamba Yesu alikuwa bila hatia. Kwa hatua hii, Pilato alijihukumu mwenyewe kwamba ana hatia, maana hakuwa na ruhusa hata kumpiga mkamatwa asiye na hatia.

Wayahudi walijua sana kwamba sheria ya kirumi iliwakataza kumwua yeyote, na kwamba Pilato angewashambulia wao, kama wangefanya hivyo kinyume cha matamshi yake ya kuhakikisha kutokuwa na mawaa. Sheria za kiyahudi haikuwa na tamko la kusulibisha, ila kwa kumpiga mtu kwa mawe. Walivyoona wao Yesu alitamka ya unajisi na hivyo kustahili kupigwa kwa mawe afe.

Wazee wa wayahudi walielewa kwamba, kama madai ya Kristo kuwa Mwana Mtukufu ndiyo kweli, basi ingewapasa kuinama mbele zake. Kusulibishwa kwake „kungethibitisha“ kwamba yeye siye tukufu pamoja na mateso yote aliyoyavumilia. Hivyo wao wangetakata kwa kufa kwake - siyo kwa damu inayoridhisha - bali kwa kifo mtini tu iliyopatana na thibitisho la Mungu.

Sala: Bwana Yesu, tunakushukuru kwa ajili ya maumivu na mateso uliyoyavumilia, uliyapokea mapigo yetu. Twakutukuza kwa ajili ya uvumilivu wako, upendo na enzi. Wewe ndiwe Mfalme wetu. Utusaidie kukutii; tufundishe kuwabariki adui zetu na kuonyesha huruma na kwao wanaotuchukia. Tunakusifu kwa sababu damu yako inatakasa makosa yetu. Ee Mwana wa Mungu, sisi tu wako. Tuweke msingi ndani ya utukufu wako, ili tutembee kwa huruma, na tukiwa na shukrani kwa ajili ya mahangaiko yako.

Swali 113: Tunajifunza nini kwa picha ya Jesu akipigwa, kuvaa vazi la zambrau na taji ya miiba ?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on June 18, 2017, at 08:31 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)