Home
Links
Bible Versions
Contact
About us
Impressum
Site Map


WoL AUDIO
WoL CHILDREN


Bible Treasures
Doctrines of Bible
Key Bible Verses


Afrikaans
አማርኛ
عربي
Azərbaycanca
Bahasa Indones.
Basa Jawa
Basa Sunda
Baoulé
বাংলা
Български
Cebuano
Dagbani
Dan
Dioula
Deutsch
Ελληνικά
English
Ewe
Español
فارسی
Français
Gjuha shqipe
հայերեն
한국어
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
Кыргызча
Lingála
മലയാളം
Mëranaw
မြန်မာဘာသာ
नेपाली
日本語
O‘zbek
Peul
Polski
Português
Русский
Srpski/Српски
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
ไทย
Tiếng Việt
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Uyghur/ئۇيغۇرچه
Wolof
ייִדיש
Yorùbá
中文


ગુજરાતી
Latina
Magyar
Norsk

Home -- Kiswahili -- John - 060 (The devil, murderer and liar)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
1. Maneno ya Yesu kwenye sikukuu ya Vibanda (Yohana 7:1 – 8:59)

f) Ibilisi, mwuaji na mwongo (Yohana 8:37-47)


YOHANA 8:44
“Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tama za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa sababu hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.”

Yesu humweleza kila mtu asiyempenda kwamba, baba yake ni Ibilisi. Kwa njia hiyo aliwaonyesha ukweli juu yao wenyewe, ingawa walidai kumjua Mungu. Hao wanasheria walikuwa mbali na Mungu. Huyu Mwovu ndiye alikuwa mzazi wao.

Ibilisi hutokeza vurugo kote aendako. Shabaha yake ni kuangusha uumbaji wa Mungu. Anachunguza apate sehemu za udhaifu ndani ya kila mtu, akijaribu kwa ujanja apate kumtawala kwa kumsukuma mtu atende dhambi. Ndipo anawahi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, akimshitaki yule aliyeanguka dhambini; hivyo anathibitisha usawa wa adhabu ya Mhukumu yuu ya fukara - ndiyo ubaya wa udanganyifu wake!

Yesu alimweleza Shetani kuwa ndiye jumla ya tamaa mbaya, iliyomwondolea nafasi ya kutaka mema. Akawa mtumwa wake mwenyewe, akimchukiza mtu yeyote. Katika roho iyo hiyo waliishi maadui wa Yesu wote, wakiwaharibu wengine na wenyewe pia, wakisukumwa na tamaa zao. Wote waishio mbali na Bwana wanaegemea ubaya ambayo Shetani anachochea ndani yao.

Tamaa za Shetani ni zipi? Yesu hutueleza kwamba yeye ni mwuaji tangu mwanzo; hii ni kwa sababu anachukia kabisa mfano wa Mungu ndani ya mtu. Yeye naye alijitenga na Mungu, aliye Mtoa-Uzima. Ndani yake kifo cha milele kimekamilika. Yeye akawa mwenye enzi ya kifo. Shabaha yake ni kufuta kabisa vyumbe vyote wenye uhai.

Asili ya ukatili huo ni udanganyifu. Ibilisi alidanganya mume na mke wa kwanza kwa kusema uongo kwa Adamu na Hawa wasiamini na kuvuka agizo la Mungu. Yeye naye alijizuzua mwenyewe alipokuwa akisimamia jeshi la malaika, alipojidhania kuwa mkubwa zaidi, mzuri zaidi na mwenye nguvu zaidi ya Mungu.

Kujidanganya hivyo ndiyo asili ya Shetani, alipokosa kutambua mipaka ya uwezo wake, na hivyo kuanguka kwenda chini kabisa. Kristo ndiye aliye kinyume kabisa na hali hiyo. Yeye ni mnyenyekevu na bila kiburi. Inahuzunisha kwamba mwanadamu hupendelea madanganyo na kuringa kuliko unyenyekevu wa Kristo na namna alivyojinyima. Hivyo mdanganyi anakusanya jeshi la waongo, ambao midomo yao hutokeza maneno ya uongo, sawa na nyoka wanaotia sumu kwenye uhai. Tena hakuna kutegemeana wao kwa wao.

Mwanamke fulani alisema kwa mamaye, „Wote ni waongo; wanajipendekeza wao kwa wao wakicheka. Kila mmoja anajiheshimu mwenyewe tu; wanafunzi wanadanganya wakati wa mitihani; wafanyi biashara hudanganya. Hata manyumbani udanganyifu hufanyika kati ya mume na mke. Hakuna amtegemeaye mwenzake, ila kila mmoja anajihesabia kuwa yeye tu ni mtu mnyofu.“

Uchokozi wa Shetani ni maongo! Mara nyingi maongo hayo yanayo ukweli wa nusu nusu. Shetani hutengeneza kila uongo isikike sawa na tamu. Yeye ndiye Mdanganyi na baba wa uongo wote.

YOHANA 8:45-47
“Nami, kwa sababu nasema iliyo kweli, hamnisadiki. Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki? Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.”

Yesu pekee husema kweli, naye hufunua kweli ya Mungu. Na wabarikiwe wale waaminio maneno yake. Yeye hutambua ukweli wa ulimwengu wote, lakini akawa mnyenyekevu na mwaminifu katika yote asemayo.

Wengi hawakubali wakati mwema wa ukweli huo, kwa sababu ni Yesu anayeitamka. Ikiwa kiongozi wa siasa au msimamizi wa kidini angetamka hayo aliyotamka Yesu, watu wangemwamini. Lakini Yesu aliposema kama mtu wa kawaida, watu walimkatalia waziwazi, kwa sababu wanatamani ukuu na kutawala wengine, kuliko hali ya unyenyekevu.

Yesu aliwauliza Wayahudi kinaganaga, “Kwa nini hamniamini? Mmeona udanganyifu au kiburi ndani yangu au nikiongoza mambo ovyo? Hapana, wakati wote nasema kweli na kuishi hivyo. Mimi ndimi Kweli mwilini, bila kosa, mnyofu pasipo hila au uongo.”

Mwishowe Yesu aliwatangazia watu wake wenye ukaidi, “Yeye aliye wa Mungu atasikia maneno yake na kutambua sauti yake. Jinsi mtoto anavyoweza kutofautisha vizuri sauti ya mzazi wake mbali na sauti za wengine. Mama naye, anaopsikia kilio cha mtoto wake mchanga, atamkimbilia. - Basi, ndivyo waitwa wa Mungu wanasikia sauti ya Baba yao wa mbinguni; lakini wale wanaoshindwa kutambua maneno ya Injili, hao sio wa Mungu. Mtu aweza kuwa mcha Mungu, akisali na kufunga, hata hivyo yawezekana kwamba, baba yake ni ibilisi. Kicho tu peke yake hakituokoi, bali kuzaliwa mara ya pili kwa damu ya Kristo, ili Roho aweze kutujalia na kudumu ndani yetu. - Basi, nani ni baba yetu, Mungu au Shetani? Usiwe na haraka kwa kujibu, bali ulinganishe makusudi yako na yule Mwenye Uovu; ndipo linganisha na kazi za Kristo zilivyo safi, halafu ukatubu.”

SALA: Ee Baba wa mbinguni, twakushukuru kwa kutufundisha ukweli juu ya dhambi zetu na juu ya upendo wako. Nisamehe maongo yangu, na uniweke huru na chuki zote na kiburi. Uninyakue toka kwa nguvu ya Shetani; hivyo niweze kujinyima na nisiendelee katika hatua za kujidanganya mwenyewe. Fungua masikio yangu na moyo wangu kwa Injili yako, na unifanye niwe mnyenyekevu na mwaminifu.

SWALI:

  1. Tabia za ibilisi ni zipi, ambazo Yesu alitufunulia waziwazi?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:18 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)